Mbaazi za nazi.#local ingredients contest

Source : Pasua Nazi Yako Kuna Kwa Kutumia Mbuzi Kamua Kutoa Tui La Kwanza Na La Pili Weka Mbaazi Zako Zilizochemshwa Tayari Andaa Mahitaji Yako L Tayari Kwa Ku...

PreTime
more Minutes
CookTime
a few Minutes
Yield
Some Servings

Sent by

at : November 7, 2025

Step:

  1. Pasua nazi yako, kuna kwa kutumia mbuzi.Kamua kutoa tui la kwanza na la pili.

    Mbaazi za nazi.#local ingredients contest recipe step 1 photo
  2. Weka mbaazi zako zilizochemshwa tayari.

    Mbaazi za nazi.#local ingredients contest recipe step 2 photo
  3. Andaa mahitaji yako.l, tayari kwa kupika.

    Mbaazi za nazi.#local ingredients contest recipe step 3 photo
  4. Weka kitunguu kwenye sufuria,tia mafuta ya kutosha kisha pika kwenye moto mdogo taratibu.

  5. Kitunguu kisiunguee* weka saumu yako uliotuangaa kisha koroga.

  6. Pika kwa dakika moja ukiweka maji kuzuia kuungua.

  7. Weka nyanya zako na chumvi ya kutosha,koroga,funika na pika kwa dakika 2.

  8. Koroga,Pima vijiko 2 vidogo vya Curry powder na uweke kwenye nyanya,koroga kwa sekunde kadhaa.

  9. Chukua mbaazi zako, hakikisha ni Kavuu bila yale maji ya kuchemshia,weka kwenye mchanganyiko wako na ukoroge bila kuacha.Utanzaa kuona mabaazi zinakuwa na uzito....sio moja moja tena.

  10. Chukua hoho yako na uweke (naweka hoho hapa ili ladhaa yake kwenye chakula iwepo)weka na Pilipili yako.

    Mbaazi za nazi.#local ingredients contest recipe step 10 photo
  11. Chukua tui la nazi lile la pili mimina,koroga na ufunike.Funua pale linakaribia kukaukia.

  12. Weka tui lile zito la kwanza,koroga,funika na uepue baada ya dakika 15.

  13. Weka dania.Tayari kwa kupakua.


Ingredients

  1. 500 g mbaazi(pegion peas)
  2. 2 Vitunguu
  3. 1 Hoho
  4. 2 Nyanya
  5. 3 Saumuu vipande
  6. Chumvi
  7. Nazi moja
  8. Curry powder
  9. Mafuta
  10. 1 Pilipili
  11. Dania

Related Recipes

Dengu samosamanda recipe

Dengu samosamanda recipe

Moist EGGLESS Choco n coffee CAKE

Moist EGGLESS Choco n coffee CAKE

Viazi karai

Viazi karai

Mbaazi za nazilocal ingredients contest

Mbaazi za nazilocal ingredients contest

Spicy githeri4weekschallenge

Spicy githeri4weekschallenge

Half cakes

Half cakes

Fried sweet banana dumplings

Fried sweet banana dumplings

Microwave-Chocolate mug cake

Microwave-Chocolate mug cake