Source : Pasua Nazi Yako Kuna Kwa Kutumia Mbuzi Kamua Kutoa Tui La Kwanza Na La Pili Weka Mbaazi Zako Zilizochemshwa Tayari Andaa Mahitaji Yako L Tayari Kwa Ku...
PreTime
more Minutes
CookTime
a few Minutes
Yield
Some Servings
Sent by Beritha Mtei
at : November 7, 2025
Step:
Pasua nazi yako, kuna kwa kutumia mbuzi.Kamua kutoa tui la kwanza na la pili.
Weka mbaazi zako zilizochemshwa tayari.
Andaa mahitaji yako.l, tayari kwa kupika.
Weka kitunguu kwenye sufuria,tia mafuta ya kutosha kisha pika kwenye moto mdogo taratibu.
Weka nyanya zako na chumvi ya kutosha,koroga,funika na pika kwa dakika 2.
Koroga,Pima vijiko 2 vidogo vya Curry powder na uweke kwenye nyanya,koroga kwa sekunde kadhaa.
Chukua mbaazi zako, hakikisha ni Kavuu bila yale maji ya kuchemshia,weka kwenye mchanganyiko wako na ukoroge bila kuacha.Utanzaa kuona mabaazi zinakuwa na uzito....sio moja moja tena.
Chukua hoho yako na uweke (naweka hoho hapa ili ladhaa yake kwenye chakula iwepo)weka na Pilipili yako.
Chukua tui la nazi lile la pili mimina,koroga na ufunike.Funua pale linakaribia kukaukia.
Weka tui lile zito la kwanza,koroga,funika na uepue baada ya dakika 15.